UONGOZI SIMBA WASEMA HAYA KUHUSU MKUTANO WA JUMAPILI

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba mkutano wao wa siku ya jumapili ya desemba 3 mwaka huu uko palepale,mkutano ambao utakuwa na agenda moja tu ya kumtangaza mshindi aliyeshinda tenda ya dhabuni ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba.

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kwamba mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Nyerere kuanzia mishale ya saa nne asubuhi huku zoezi la uandikishaji likianza saa mbili asubuhi kwa wanachama wote.

Manara alisema kwamba mkutano huo ni muhimu kwa klabu ya Simba,kwani utakwenda kubadilisha histolia ya muundo wa klabu,hivyo ni vyema wanachama wakajitokeza kwa wingi katika mkutano huo.

Aidha Manara alisema kwamba klabu ya Simba imepokea taarifa kutoka TFF inayozungumzia kanuni ambazo zimetolewa na Wizara ya michezo juu ya mchakato huo wa mfumo wa mabadiliko ya ya muundo wa uendeshaji wa timu.

Alisema kwamba uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa kaimu rais wake,Salim Abdalah ulikwenda kufanya mazungumzo na wizara ambapo mazungumzo hayo yanaendelea na lengo kuu ni kuziboresha hizo kanuni ili kila mmoja aweze kufaidika.

No comments