KILIMANJARO STARS TAYARI KWA SAFARI YA KENYA

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania bara,Kilimanjaro Stars hapo kesho kinataraji kuelekea nchini Kenya kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya kombe la Challenge itakayoanza desemba 3 mwa ka huu.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kikosi hicho kinataraji kusafiri kwa ndege ya shirika la Kenya KQ hapo kesho kunako mishale ya saa nane mchana.

Lucas alisema kwamba kikosi kitafiki uwanja wa ndege wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kuanzia mishale ya sita huku kocha mkuu Ammy Ninje atakuwepo hapo mapema zaidi kuanzia mishale ya saa tano asubuhi ili aweze kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya safari.

Alisema kwamba hali ya kikosi iko vizuri na kila mchezaji ana morali ya kwenda kuifanyia vyema nchi katika michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya ukanda wa Afrika mashari na kati CECAFA.

No comments