AZAM FC WAFUNGA ZOEZI LA USAJILI

Uongozi wa klabu ya Azam FC,umesema kwamba kwa sasa wameshafunga rasmi zoezi la usajili katika klabu hiyo baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji Bernard Arthur kutoka nchni Ghana.

Afisa Habari wa timu ya Azam FC,Jafari Idd amesema kwamba kwa mujibu wa lipoti ya kocha mkuu wa timu hiyo kwa sasa hakuna mapendekezo yoyote ya usajili yanayohusiana swala la kuongeza mchezji ndani ya klabu hiyo.

Jafari alisema kwamba mbali na swala la kutoengeza wachezaji lakini pia hakuna mchezaji atakaeachwa katika dirisha hili dogo la usajili.

No comments