KAMUSOKO AFANYIWA VIPIMO ILI KUNUSURU GOTI LAKE

Na Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umechukua jukumu la kumpatia matibabu ya juu kiungo wa timu hiyo Thabani Kamosoko anaesumbuliwa na majeraha ya goti kwa muda mrefu.

Ili kuhakikisha mchezaji huyo anarejea katika hali yake nzuri na kuendelea kuitumikia timu hiyo,uongozi umechukua jukumu la kumpleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa vipimo zaidi.

Kamusoko kwa muda mrefu ameshindwa kuisaidia timu yake katika michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Tanzania bara baada ya kusumbuliwa na matatizo ya goti ambayo yamemfanya kushindwa kabisa kurejea uwanjani.

No comments