ALLY BUSHIRI KUIONGOZA POLISI TANZANIA

Na,Sleiman Ussi,Unguja
Kocha wa zamani wa timu ya Mwadui FC,Ally Bushiri maarufu kwa jina la "The Big Boss"amethibitisha taarifa za yeye kujiunga na klabu ya Polisi Tanzania ambayo inashiliki ligi daraja la kwanza kwa ajili ya kukifundisha kikosi cha timu hiyo.

Bushiri alisema kwamba amefikia makubaliano na uongozi wa Polisi Tanzania kwa ajili ya kwenda kukisaidia kikosi cha timu hiyo ili kifanikiwe kupata nafasi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

Alisema kwamba yeye atakuwa na kazi moja ya kusimamia mechi za timu hiyo ambazo zimesalia na baada ya hapo kama kutakuwa na maelewano mazuri basi atasaini kandarasi ya moja kwa moja kwa ajili ya kuwafundisha maafande hao.




No comments