YANGA KUZINDUA NAMFUA STADIUM

Uongozi wa timu ya Singida United,umesema kwamba wanategemea kuutumia uwanja wao wa nyumbani (NAMFUA STADIUM) wakati wa mechi yao ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo timu ya Yanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoelezwa na uongozi wa klabu hiyo umesema kwamba hadi kufikia sasa ukarabati wa uwanja huo unaendelea vizuri na wanaamini hadi kufikia siku hiyo ya mechi ambayo itapigwa octoba 21,2017 kila kitu kitakua kimeshakamilika.

Taarifa hiyo imeeleza kua lengo la kuutumia uwanja huo ni kuwapa burudani kwa wanasingida na mikoa jirani kwa ujumla.

Singida United kwa sasa inautumia uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kama uwanja wao wa nyumbani baada ya uwanja huo wa Namfua kua katika ukarabati wa miundo mbinu.

No comments