KCB YADHAMINI LIGI KUU YA TANZANIA BARA

Benki ya KCB Tanzania leo hii imetangaza rasmi udhamini mwenza wa ligi kuu ya Tanzania bara kwa kuingia mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi za kitanzania 325,000,000.

Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari wakati wa kusainiwa mkataba huo,Rais wa TFF,Wallace Karia kwa upande wake aliishukuru benki hiyo ya KCB kwa kuidhamini ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu wa mwaka 2017/2018.

Karia pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kwa kuweza kutoa michango ya hali ya na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Benki ya KCB, Cosmas Kimario alisema kwamba udhamini huo upo ndani ya vipaumbele vya benki kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.

"Sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi nchini,hivyo benki ya KCB imechukua uamuzi huu kujiunga na TFF kukuza mchezo wa mpira wa miguu"alisema Kimario.

No comments