MANJI AELEZA SABABU ZA KUJIUZULU YANGA

Aliyekua mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Yusuph Manji mwenye umri wa miaka 41 ameithibitishia mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kua ana vyuma vitano kwenye moyo ambavyo aliwekewa katika hospitali ya India,Marekani,Dubai na Aghakani.

Manji ametoa ushahidi huo leo hii mahakamani mbele ya hakimu mfawidhi Syprian Mkeha ambapo amethibitisha kitendo cha kutuhumiwa kua anatumia madawa ya kulevya kimemdhalilisha jambo ambalo lilimsababisha kuandika barua ya kujiuzulu katika klabu ya Yanga.

Pia limemfedhehesha hata kuingia msikitini na alishindwa kwenda Hijah kutokana na tuhuma hizo.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka hosptali ya Aghakani,DK Mustapha amethibitisha Manji kua na ugonjwa sugu wa Moyo akiwa na umri mdogo na anashangaa hadi leo hii anatembea ambapo yeye ndie aliyemuwekea chuma cha tano kwenye moyo februari 24/2017.

Aidha Dk Mustapha amekili kua dawa za mofini na dayasipan zilizokutwa kwenye sampuli yake ya mkojo ni miongoni mwa dawa ambazo anazitumia kwa ajili ya maumivu makali ya mgongo na moyo.

Shauri hilo litaendelea tena hapo kesho katika mwendelezo wa ushahidi uliopangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo.

No comments