UNGOZI WA MPIRA WA KIKAPU WAFURAHISHWA NA HAMASA YA WADAU

Ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam imefanikiwa kukamilika siku ya jumamosi ambapo timu ya Savio kwa upande wa wanaume imefanikiwa kuwa mabingwa wa ligi hiyo.

Mkurugenzi wa masoko na mawasiliano wa chama cha Basketball Dar es salaam,Peter Mpangala alisema kwamba nafasi ya pili kwa wanaume imechukuliwa na JKT huku mshindi wa nafasi ya tatu imechukuliwa na vijana.

Mpangala alisema kwamba kwa upande wa wanawake,timu ya vijana Quens imefanikiwa kuwa bingwa ikifuatiwa na Don Bosco Lions na nafasi ya tatu imeshikiliwa na JKT Stars.

Alisema kwamba kiujumla ligi hiyo ya Star Times RBA ilikua na ushindani wa hali ya juu kwa timu zote pia kulikuwepo kwa hamasa kwa wapenzi wa mpira wa kikapu hasa katika fainali.

Hata hivyo aliongeza kua kwa sasa chama hicho kipo katika maandalizi ya kuandaa michuano ya Star Times Super Cup ambayo kwa kipindi kirefu yalikua hayafanyiki.

No comments