YANGA WAANZA MCHAKATO WA UJENZI WA UWANJA

Uongozi wa klabu ya Yanga tayari umeshaanza mchakato wa ujenzi wa uwanja wao uliopo Jangwani kwa ajili ya timu kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.

Afisa Habari wa timu hiyo Dismas Ten alisema kwamba kwa sasa tayari zoezi la kumwaga vifusi kwenye uwanja huo tayari limeshaanza kwa ajili ya kufanikisha mchakato huo.

"Tumeanza taratibu za awali za ujenzi wa uwanja wetu ama kurekebisha uwanja kwa sababu tunahitaji kua na sehemu nzuri tulivu kwa ajili ya mazoezi kwa hiyo taratibu za mwanzo zimeshaanza kwa wale ambao wanapata nafasi ya kupita hapa makao makuu wanaona vifusi vinamwagwa kwa maelekezo mazuri kabisa kutoka kwa wataalamu wa ujenzi"alisema Dismas.

Hata hivyo Dismas amewaomba wadau wenye uwezo waweze kuwasidia  kuwapatia vifusi kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo kwakua eneo ni kubwa na linahitaji vifusi vingi.

No comments