DAIMOND PLATINUMZ AENDELEA KUPONGEZWA

Wadau mbalimba wamejitokeza kumpongeza msanii nguli wa bongo frever Daimond Platinumz AKA Chibu Dangote kwa kitendo chake cha kumtakia heri ya kuzaliwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu.


Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram aliandika ujumbe unaosomeka "Happy Birthday Madam"akiambatanisha na picha ya Wema Sepetu akiwa na mshindi  wa big brother 2014 Idris Sultan ambae nae ni miongoni mwa waliotoka nae kimapenzi msanii huyo wa maigizo.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Daimond alipongezwa na fans mbalimbali ambao walicomenti kwenye Akaunti yake hiyo ingawa baadhi yao walilipokea jambo hilo tofauti.

Ikumbukwe kua hii ni mara nyingine Platinumz anaendelea kupongezwa baada ya siku chache zilizopita kupongezwa na mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Haule aka Profesar Jay kutokana na uamuzi wake wa kumkubali mtoto aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.

Wema Sepetu leo hii anasherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo katika mitandao mbalimbali ya kijamii wadau wengi wamejitokeza kumpongeza mrembo huyo mwenye mashabiki wengi kibongo bongo na nje ya mipaka ya nchi.

No comments