YANGA WALIMALIZA SWALA LA PIUS BUSWITA

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejipanga vyema kuwakabili Mtibwa Sugar hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Afisa Habari wa timu hiyo Dismas Ten ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba kuelekea kwenye mchezo huo watakosekana wachezaji wawili Amis Tambwe na Papy Kabamba Tshishimbi anaetumikia kadi tatu za njano huku Tambwe bado hayuko vizuri baada ya kua majeruhi tangu kuanza kwa msimu wa ligi.

Alisema kwamba swala la mchezaji Pius Buswita limeshamalizika hivyo kama benchi la ufundi litahitaji kumtumia kwenye mechi hiyo basi ni jukumu lao.

No comments