MANARA AISIFU YANGA

Mkuu wa idara ya habari katika uongozi wa klabu ya Simba,Haji Manara amesema kwamba hadi kufikia sasa klabu ya Yanga haijabebwa na waamuzi kama ilivyokua kwa msimu uliopita chini ya uongozi wa Jamali Malinzi.

Manara ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba matokeo ambayo wameyapata Yanga katika mechi nne walizocheza ni ya jitihada zao binafsi wala sio ya kupendelewa na waamuzi.

Alisema kwamba msimu uliopita Yanga ilibebwa zaidi na waamuzi na ikapelekea hadi waamuzi wengi kukumbana na adhabu za TFF ikwemo wengi wao kufungiwa.

Aidha amelitaka shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini kuhakikisha wanapanga waamuzi bora katika michezo ya ligi ili kuondoa mizozo ambayo haina msingi kwa maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

No comments