TAGOANE WAWAHIMIZA WASANII KUJIUNGA NA MTANDAO HUO

Katika kuhakikisha kuwa wasanii wa njimbo za injili wanafanikiwa kujikwamua kimaendeleo kupitia kazi zao,leo hii mtandao wa wasanii wote wa Tasinia ya Injili na maadili ya Utaifa unaotambulika kwa jina la TAGOANE umetangaza rasmi kukabidhiwa kibali kutoka kwa baraza la sanaa ambacho kibali hicho kitawafanya kufanya kazi zao kwa weledi.

Rais wa mtandao huo wa TAGOANE, Dk Godwin Maimu Nnyaka alisema kwamba moja ya malengo ya mtandao huo ni kuwaleta pamoja wasanii wote wa Tasnia ya Injili ili kuwa na sauti moja luga moja,ili kufikia malengo yao ya kiroho na kimwili.

Alisema kwamba pia TAGOANE itashirikiana na serikali katika kukuza pato la Taifa na wasanii wote kwa kudhibiti wauzaji haramu,wanyonyaji,na matapeli wa kazi za ,wasanii,kwa kuhakikisha wanadhibitiwa kwa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa ustawi wa wasanii na Taifa.

Hata hivyo aliongeza kuwaambia wasanii wa njimbo hizo kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha katika mtandao huo wa wanachama wa TAGOANE,ambapo amedai kua yoyote yule anaefanya kazi ya sanaa katika Tasnia ya injili na maadili ya Utaifa anastahili kuwepo kwenye mtandao huo.

Wahusika hao ni pamoja na Watunzi wa Tungo za nyimbo,waandishi wa vitabu,Filamu,Tamthilia,Walimu wa sanaa husika,Waimbaji,Wachezaji/dansa,wapiga ala au vyombo vya muziki,wazalishaji wa kazi za sanaa (Prodyuza),Wavumbuzi (Disigner)

Pia kuna wapiga picha za mnato na zinazotembea,wasanii wa kazi wasanii (Managers/Directors),watangazaji wa kazi zote za tasnia ya sanaa ya injili,wachekeshaji,kwaya Band,vikundi vya ngoma na sanaa za asili pamoja na wasambazaji wa kazi za sanaa nk.

No comments