NYAMBAYA AWATOA HOFU WADAU WA MPIRA SWALA LA USIMBA NA UYANGA NDANI YA TFF
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF kanda ya Dar es salaam,Lameck Nyambaya amesema kwamba kuelekea katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara kwa upande wao kama uongozi umejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa ligi inakuwa bora ambayo itatizamwa sehemu mbalimbali.
Nyambaya alisema kwamba hata swala la kupanguliwa kwa ratiba ya ligi, kwao swala hilo wameliwekea uzito wa hali ya juu na wameshatoa taarifa kwa uongozi wa bodi ya ligi kulipatia ufumbuzi jambo hilo ili kusiwe na mvurugano wa ratiba.
Aidha alisema kwamba kwa upande wake kama muwakilishi wa kanda ya Dar es salaam atahakikisha mapato ambayo yatapatikana katika kanda yake vilabu shiriki vipata stahiki zao bila kikwazo.
Hata hivyo aliongeza kwa kuwatoa hofu wadau wa mpira wa miguu hapa nchini kuondoa dhana ambayo imeanza kuzungumzwa na baadhi ya wadau wa mpira wa miguu hapa nchini kuwa TFF inaendeshwa kwa mfumo wa Usimba na Uyanga,ambapo amedai swala hilo halipo kwani viongozi wote waliochaguliwa wanafahamu vizuri taratibu za uendeshaji wa mchezo huo unaopendwa zaidi ulimwenguni.
Post a Comment