EMMANUEL OKWI AISIFU YANGA

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Simba,Emmanuel Okwi amesema kwamba mchezo wa jana wa ngao ya jamii uliowakutanisha Simba na Yanga ulikuwa mchezo mgumu zaidi ambao amewai kushiriki.

Okwi alisema kwamba kwao hawakutegemea kama Yanga wangeleta upinzani wa hali ya juu kama ambavyo waliuonyesha katika mchezo huo,hivyo kushinda kwao kwa changamoto ya mikwaju ya penati na jambo la kushukuru.

Alisema kwamba Yanga ilicheza vizuri katika pambano hilo na anaamini katika ushiriki wa ligi kuu ya Tanzania bara kutakuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na ubora wa vikosi vyote.

No comments