YANGA WANASUBIRI BARUA YA TFF KUTOA MAAMUZI YA BUSWITA

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga umesema kwamba kwa sasa wanasubiri barua kutoka TFF ili klabu hiyo itoe taarifa yao rasmi juu ya kufungiwa kwa mchezaji wao Pius Buswita sambamba na hatma ya mchezaji Obrey Chirwa.

Afsa Habari msaidizi wa timu hiyo,Godilsten Anderson Chicharito alisema kwamba hadi kufikia sasa bado hawajapata barua rasmi inayoeleza swala hilo la kufungiwa mwaka mmoja mchezaji wao aliyesajiliwa kutoka klabu ya Mbao FC ya Ilemela mkoani Mwanza.

Alisema kwamba uongozi kwa sasa hawana taarifa rasmi juu ya maamuzi hayo ya kamati,hivyo kilichopo wanasubiri kupata barua rasmi ili na wao waeleze mtazamo wao juu ya jambo hilo.

Aidha Chicharito alisema kwamba hata swala la mchezaji Obrey Chirwa nalo uongozi uko mbioni kuiandikia barua TFF ili kujua nini kinaendelea kwa mchezaji huyo baada ya kusimamishwa na TFF huku shirikisho hilo likishindwa kuweka bayana juu ya ukomo wa adhabu yake.

No comments