TFF YABADILI MUDA WA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limefanya mabadiliko ya muda katika mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga unaotarajiwa kupigwa agost 23 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Afsa habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba pambano hilo sasa litapigwa saa 11 jioni kwa saa za Afrika Mashari badala ya saa kumi kamili jioni.

Lucas alisema kwamba maamuzi hayo yamefanyika baada ya pande zote kukubaliana na jambo hilo ambalo lina nia ya kuwapa fursa wadau waweze kulishuhudia pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

No comments