KESI YA MANJI YA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YAANZA KUSIKILIZWA

Na Unique Maringo
Mashahid wawili kutoka kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai kanda maalumu Dar es salaam,wameanza kutoa ushahidi wao katika kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya inayomkabili aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yisufu Manji.

Wakitoa ushahidi wao mbele ya Hakimu mfawidhi Mahakama ya Kisutu Cyprian Mkeha,wakiongozwa na mwendeshamashtaka wa serikali Timon Vitalisi,shahidi No moja Ramadhani Kings 42 ameileza Mahakama kuwa yeye ni Afsa upelelezi makosa ya jinai ofisi ya kanda maalumu ya Dar es salaam.

Alisema mnamo February 9/2017 alipokea ripoti kutoka kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai ya kumhusisha Yusufu Manji na madawa ya kulevya.

Ambapo siku hiyo alimpokea mtuhumiwa Yusufu Manji na Josephati Gwajima.

Shahidi ameendelea kudai kuwa sikuhiyo watuhumiwa hao walifika Polisi kuripoti ambapo alipokea taarifa ya kumtaka awapeleke watuhumiwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kujua kama watuhumiwa wanatumia madawa ya kulevya na aliwakabidhi watuhumiwa kwa dictetive coplo sosipita ambapo agizo lilitekekelezwa.

Ameongeza kua baadae taarifa zilikuja Gwajima hatumii ila Yusu Manji kwenye Sampuli ya mkojo kimekutwa Dawa za kulevya aina ya Benzodiazpan.

Baada ya kupata tarifa hizo walipeleka jalada kwa Dpp kwa ajili ya upelelezi na hatimae mshtakiwa kufikishwa mahakamani.

Kwa upande wake wakili upande wa utetezi Hudson Ndusypo alipo mtaka shahidi kuithibitishia mahakama kuwa kama walimpatia Manji msaada wadawa wakati akiwa chini ya ulinzi shahidi amekiri kuwa ni kweli.

Ndusyepo alipohojiwa endapo mtuhumiwa angekataa kutoa kutoa mkojo nini kongefuata wakati alikua chini ya ulinzi wake amejibu hakuna chochote kingetokea.

Wakili amehoji kuwa walipo fika nyumbani kwa Manji moja ya vitu walivyo chukua ilikua ni Dawa aina ya valiam ambazo zilikua chumbani kwake ambapo shahidi amejibu vilivyopatikana havihusiani na ishu za madawa ya kulevya.

Aidha shahid no 2 dictetiv coplo sosipita nae ametoa ushahidi wake kua alimpeleka mtuhumiwa kwa mkemia mkuu na sampuli ya mkojo iligundulika kua na matimizi ya Dawa ya kulevya.

Manji alifiikishwa mhakamani hapo kwa Mara ya  kwanza February 16 2017 akidaiwa kuwa kati ya February 6 na 9 2017 ktk eneo la upanga View Ilala jijin DSM alikutwa ametumia madawa ya kulevya aina ya Heroin aina ya Deazopan.

Amelikana shtaka na kuachiwa kwa dhamana ya mdhamini mmoja alie Spain bondi ya shilingi million kumi.

Shauri hilo litaendelea tena hapo kesho.

Hata hivyo Manji bado ataendelea kuwepo rumande kutokana na mashitaka yake  sita yanayoendelea kumkabili ambayo yanahusiana na uhujumu uchumi na usalama wa Taifa.

No comments