CHIRWA NA DEUS KASEKE KUIKOSA MICHEZO YA LIGI KUU

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba mchezaji wa Yanga,Obrey Chirwa na kiungo wa timu ya Singida United,Deus Kaseke hawataruhusiwa kucheza katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara hadi hapo kamati ya masaa 72 itakapokutana na kutoa maamuzi yake.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT,kwamba wachezaji hao hawatacheza katika mechi za ligi kuu bila kupata idhini ya kamati ya masaa 72 kwa sababu wachezaji hao akiwemo winga aliyeuzwa na Yanga,Simon Msuva walimsukuma mwamuzi katika mechi iliyowakutanisha Yanga na Mbao iliyochezwa jijini Mwanza msimu uliopita.

Lucas alisema kwamba wachezaji hao kwa pamoja walisimamishwa na kamati ya masaa 72 na hadi sasa bado maamuzi yao hayajatolewa na kamati hiyo.

Alisema kwamba kiungo wa Singida United,Deus Kaseke licha ya kuihama klabu ya Yanga lakini bado ataendelea kuitumikia adhabu hiyo kutokana na sheria zilizopo ndani ya shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF.


No comments