MANJI AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji anaetuhumiwa kwa kosa la kutumia madawa ya kulevya aina ya Heroin 

Hakim mfawidhi Mahakama ya Kisutu anaesikiliza shauri hilo amefikia maamizi hayo Mara baada ya kubaini kuwa upande wa mashtaka umejenga kesi yao ambayo inahitaji mshtakiwa kujitetea.

Ktk kesi hiyo upande wa mashtaka ulihitaji mashahidi wa tatu ambao ni askari wa wili na mkemia wa serikali.

Mara baada ya maamuzi hayo Wakili wa Manji Had son Ndusyepo alisema kuwa mteja  wake atajitetea kwa kiapo na ataita mashahidi kumi na tano.

Hakimu Mkeha ameahirisha shauri hilo hadi Agost 30 na 31 mwaka huu.

Manji alifikishwa mhakamani hapo kwa Mara ya  kwanza February 16 /2017 akidaiwa kuwa kati ya February 6 na 9 2017 ktk eneo la upanga View Ilala jijin DSM alikutwa ametumia madawa ya kulevya aina ya Heroin  Deazopan.ambapo alikana shtaka na kuachiwa kwa dhamana ya mdhamini mmoja aliesaini bondi ya sjiling million kumi.

No comments