MAYANGA AMREJESHA YONDANI KWENYE KIKOSI CHA STARS

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,Salum Mayanga ameita kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana mchezo unaotarajiwa kupigwa septemba 2 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es salaam.

Mayanga alisema kwamba mchezo huo upo kwenye kalenda ya FIFA na kambi ya mazoezi kwa timu ya Stars inatarajiwa kuanza rasmi hapo kesho mishale ya saa mbili usiku.

Katika kikosi hicho Mayanga amemjumuisha mchezaji wa timu ya Yanga,Cavin Yondan ambae tangu mwaka wa 2016 hawajai kuitumikia timu hiyo ya Taifa.

Alisema kwamba amechukumu jukumu la kumuita Yondani baada ya kufanya nae mazungumzo kabla ya kumita na mwenyewe ameridhia kujiunga na kikosi cha Taifa Stars.

Kikosi kamili cha wachezaji 21 ni pamoja na;

WALINDA MLANGO
1.Aishi Manula
2.Mwadini Ally
3.Ramadhani Kabwili

WALINZI
4.Gadiel Michael
5.Boniphace Maganga
6.Abdi Banda
7.Kelvin Yondani
8.Salim Mbonde
9.Erasto Nyoni

VIUNGO WA KATI
10.Himid MAO
11.Hamis Abdalah
12.Mzamiru Yasin
13.Said Ndemla

VIUNGO WA PEMBENI
14.Simon Msuva
15.Shiza Kichuya
16.Farid Mussa
17.Morel Ergenes

WASHAMBULIAJI
18.Raphael Daud
19.Kelvin Sabato
20.Mbwana Samata
21.Elias Maguli.

No comments