PAWASA AZIPONGEZA SIMBA NA YANGA

Aliyewai kuwa mchezaji wa timu ya Simba pamoja na timu ya Taifa ya Tanzania,Boniphace Pawasa amevipongeza vilabu vya Simba na Yanga kwa kuendelea kufanya usajili mzuri ambao anaamini utakuwa na tija kwa upande wao.

Pawasa alisema kwamba vikosi vya timu hizo vilikuwa na ufinyu wa wachezaji kwa misimu ya nyuma ambao uliwafanya kushindwa kucheza vizuri kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa.

Alisema kwamba anaamini kwa usajili uliofanywa na timu hizo huenda ukawa na chachu ya mafanikio kama makocha watapanga program zao kwa weledi kweny michuano mbalimbali.

Hata hivyo aliongeza kuwa mbali na kuwa na vikosi vipana lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo muda wa maandalizi kwa mabenchi ya ufundi ambao kunaweza kuleta athari kwa timu.

No comments