MSUVA KWENDA MOROCCO SIKU YA JUMATANO

Mchezaji wa timu ya Yanga SC, Simon Msuva anatarajiwa kuondoka nchini wakati wowote kuanzia sasa kwenda Morocco kwa ajili ya kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na klabu ya Difaa Hassani El-Jadida ya Ligi Kuu ya nchini humo.

Afisa habari wa klabu ya Yanga Dismas Ten aliiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba  Msuva  anatarajia kuondoka hapa nchini wakati wowote kuelekea huko nchini morocco kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya na endapo kama atafuzu vipimo hivyo  atasaini moja kwa moja mkataba wa kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Morroco.

Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa mchezaji huyo anataraji kuanza safari siku ya jumatano kwa ajili ya kwenda kukamilisha mchakato huo wa usajili.


No comments