YANGA WASEMA HAYA KUHUSU USAJILI WA PAPY KABAMBA TSHISHIMBI

Uongozi wa timu ya soka ya Yanga,umesema kwamba bado hawajakamilisha usajili wa mchezaji Papy Kabamba Tshishimbi kutoka katika klabu ya Mbabane Swallows licha ya mchezaji huyo kuwasili hapa nchini.

Afsa Habari msaidizi wa Yanga,Godlisten Anderson Chicharito aliambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kwa sasa viongozi wa kamati ya usajili bado wapo kwenye mazungumzo na mchezaji huyo ambapo wakati wowote watakapokamilisha usajili wake basi uongozi utatoa taarifa kwa wanachama wake.

No comments