KALLY ONGALAH KUACHANA NA MAJIMAJI

Kocha wa timu ya Majimaji ya Songea Kally Ongala amesema kwamba huenda msimu ujao asionekane katika kikosi cha timu hiyo,hii inatokana na uongozi wa klabu hiyo kushindwa kufanya maandalazi mapema kabla ya kuanza ligi.

Ongala alisema kwamba hadi kufikia sasa bado kikosi hicho hakijaanza maandalizi wala kufanya usajili mzuri ambao ungekuwa na tija kwa upande wake katika ufundishaji wa timu hiyo.

Alisema kwamba anaamini wiki ijayo ataweka bayana msimamo wake juu ya klabu hiyo lakini anaamini msimu ujao hatakuwemo kwenye kikosi cha Majimaji kama kocha mkuu.

No comments