SAID MAULID AWAPA NENO WANAOTAKA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Mchezaji wa zamani wa timu ya Simba,Yanga na Timu ya Taifa, Said Mauld amewataka wacheza waliopata nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika nchi za nje kutambua huko waendako watakutana na changamoto mpya ambapo wasipokuwa makini wanaweza kujikuta mipango yao inafel.

Maulid alisema kwamba unapocheza soka nchi za nje unakutana changamoto mbalimbali ambazo kwa mchezaji inatakiwa ukabiliane nazo Kama unahitaji kufanikiwa.

Alisema kwamba moja ya sababu ambazo watakutana nazo ni ubaguzi na kuwepo kwa makundi ambapo kwa vitendo hivyo njia moja wapo inayotakiwa kufanywa na wachezaji wetu ni kucheza kwa juhudi zaidi ili mashabiki wakubali kiwango chako. 

No comments