TAKUKURU YAWATIA NGUVUNI WADAU WA MPIRA WA MIGUU

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Mwanza imethibitisha kuwashikilia wanafamilia wa soka wakiwemo Shafii Dauda,Almas Kasongo,Elias Mwanjali,katibu wa chama cha soka mkoa wa Mwanza,mwenyekiti wa Mbeya,Lugola kutoka Shinyanga na wajumbe wa mikoa ya jirani kwa sababu ya kubaini kuwepo kwa viashiria vya rushwa na kampeni.

Mkurugenzi wa TAKUKURU,mkoani Mwanza Ernest Makale amethibitisha tukio hilo la wanafamilia hao wa soka kushikiliwa tokea siku ya jana na kuachiwa leo hii kwa dhamana.

Makale alisema kwamba taasisi hiyo bado inaendelea kulifuatilia swala hilo na litakapokamilika wataweka bayana ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

No comments