WAMOROCCO WAKAMILISHA USAJILI WA MSUVA

Winga mahili wa timu ya Yanga,Simon Msuva leo hii amejiunga rasmi na klabu ya Difaa Hassan EL Jadidi ya nchini Morocco baada ya kusaini kandarasi ya miaka mitatu kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco.

Msuva aliyeambatana na wakala wake Jonas Tiboroha amesaini mkataba huo baada ya kufuzu vipimo vya afya.

Klabu ya Yanga ilimuidhinisha winga huyo kujiunga na Difaa baada ya pande zote tatu kukubaliana kwenye maswala ya usajili ikiwemo taratibu za kifedha.

No comments