JAMALI MALINZI AWAPA NENO WAGOMBEA WA UCHAGUZI MKUU WA TFF


Rais wa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,Jamali Malinzi amewatakia kila la heri wajumbe wote wa mkutano mkuu wa TFF katika kuelekea kwenye zoezi la uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotaraji kufanyika mwezi wa nane huko mkoani Dodoma.

Katika taarifa hiyo ya Malinzi iliyotumwa na mawakili wake kampuni ya Rwegoshora inaeleza kuwa yeye ana imani kubwa kuwa uongozi utakaochaguliwa utaangalia namna nzuri ya kutilia mkazo katika mambo muhimu katika soka letu,hususani maendeleo ya soka la vijana na lile la wanawake.

Aidha ametoa shukrani za dhati kwa serikali chini ya uongozi wa John Pombe Magufuli,wadhamini mbalimbali na washirika wa TFF na  wadau wote kwa ushirikiano walioutoa kwa TFF wakati wote wa kipindi cha uongozi wake.

Wakili Domissian Rwegoshora kwa upande wake amekili kampuni hiyo kutoa maelezo ya mteja wake Jamali Malinzi.

No comments