YANGA YAENDELEA KUJIFUA MKOANI MOROGORO

Uongozi wa timu ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea vyema na maandalizi kikiwa mkoani Morogoro tayari kwa ajili ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Afsa Habari wa timu hiyo,Dismas Ten alisema kwamba wachezaji wote waliopo kambini wako vizuri na kila mmoja ana hamasa ya kujituma katika mazoezi hayo ya siku kumi wakiwa mkoani humo.
Aidha alisema kwamba mchezaji Donald Ngoma amerejea hapa nchini siku ya jana tayari kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi hayo ya ligi kuu.

No comments