KAGERA SUGAR WAKARIBISHA OFA KWA MBARAKA YUSUF

Uongozi wa timu ya soka ya Kagera Sugar umesema kwamba bado hawajapata ofa yeyote inayohusiana na usajili wa mchezaji Mbraka Yusufu anayewindwa na vilabu mbalimbali vya hapa nchini.

Mwenyekiti wa klabu hiyo Hamisi Madaki alisema kwamba uongozi uko radhi kumuachia mchezaji huyo kwa timu itakayomuitaji ispokuwa inatakiwa kufuata taratibu husika za usajili kwani mchezaji bado ana mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja.

Madaki alisema kwamba kwa sasa hawana wasiwasi na mchezaji huyo kwani mkataba wake unafahamika kwamba bado ni wa muda mrefu hivyo amezitaka timu ambazo zinataka kumrubuni mchezaji huyo wafahamu swala hilo kwamba bado ni mali ya Kagera Sugar.

No comments