SIMBA WAJINASIBU KUIVURUGA AFRIKA LYON

Mratibu wa timu ya Simba,Abasi Ally amedai kuwa kikosi cha timu hiyo kina nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara hapo siku ya jumapili dhidi ya Afrika Lyon.
Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT,Abasi alisema kwamba kwa jinsi walivyojianda kuelekea kwenye mechi hiyo anaimani Afrika Lyon haitakuwa na nafasi ya kufurukuta mbele yao kwani wamedhamiria kushinda mechi zao zote zilizosalia.

Alisema kwamba ingawa wanapokutana na Afrika Lyon huwa kunakuwa na upinzani mkali lakini kuelekea kwenye mechi hiyo ya jumapili itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam hawategemei kuwepo kwa hali hiyo.

Aidha alisema kuwa wachezaji wote wako vizuri hakuna yeyote aliye majeruhi kuelekea kwenye pambano hilo jambo ambalo linatoa nafasi kwa benchi la ufundi kumpanga yule aliye kwenye mipango yao.

Simba kwa sasa wanaendelea kushika nafasi ya kwanza wakiwa na alama 59 baada ya kushuka dimbani mara 27 huuku wakisaliwa na mechi tatu kabla ya kumaliza ligi.

No comments