MBWANA SAMATA AGUSA HISIA ZA WAZUNGU

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania,Mbwana Samata kwa sasa ameendelea kukubalika na mashabiki wa timu yake ya KR Genk ya nchini Ubelgiji baada ya baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuonyesha mapenzi ya waziwazi kwake.

Mmoja wa mashabiki wa Genk alionekana akibeba bango lenye ujumbe wa kuomba jezi ya Mbwana Samata katika moja ya mechi iliyoshiriki timu hiyo.

Samata kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha timu hiyo na mara nyingi amekuwa akizitendea haki nafasi anazozipata hasa katika ufungaji.


No comments