MWAMBUSI AWASIFU WACHEZAJI WAKE

Kocha msaidizi wa timu ya soka ya Yanga Juma Mwambusi amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma zaidi na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Mwambusi alisema kwamba mchezo wa hii leo ulikuwa mgumu zaidi kwani wapinzani wao wameonekana kucheza  kwa tahadhari kubwa hasa katika kipindi cha kwanza hivyo mabao ya Amisi Tambwe na Obrey Chirwa yamewapa faraja katika mechi ya leo.


"Napenda kumshukuru mungu kwanza lakini vilevele nawapongeza wachezaji wote lakini wachezaji wetu wamejitahidi sana,tumetoka kufungwa kwenye mechi ya FA na timu kama unavyojua ukishapoteza mchezo mnapokuja mechi inayofuata inakuwa imebadilika tofauti na mnavyotegemea"alisema Mwambusi.

Aidha alisema kwamba baada ya ushindi wa mechi ya leo kwa sasa wanajipanga kufanya vyema kwenye mechi zao nne zilizosalia ili kutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Yanga leo hii imefanikiwa kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na alama 59 sawa na Simba lakini Yanga wana faida ya kuwa na idadi kubwa ya magoli ya kufunga.

No comments