KAULI YA UONGOZI WA YANGA JUU YA MPANGO WA KUWAACHA WACHEZAJI
TAARIFA KWA UMMA
Katibu mkuu Yanga SC anapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na wadau wa soka nchini kuhusiana na taarifa mbalimbali zinazoendelea katika mitandao ya kijamii na vituo vya redio kuhusu klabu hii kuwa na mpango wa kuwaacha baadhi ya wachezaji.
Taarifa hizo ni za uongo na uzushi mkubwa,uongozi upo bega kwa bega na wachezaji wote 27 na benchi lao la ufundi. Hatujakaa kulijadili hilo wala kulifikiria bali tupo makini kutetea ubingwa wetu wa ligi kuu.
Katibu anasisitiza wachezaji wote ni muhimu na uongozi unajivunia kwa moyo wao thabiti kuitumikia klabu . Wanawaomba kuwapuuza watoa habari feki za klabu na wao kupiga kazi yao kwa umakini pia wanachama na wapenzi wa klabu msiziamini propaganda hizo zenye nio mbaya kutuvuruga.
Katibu anasisitiza ; mwenye maamuzi ya mwisho juu ya huduma ya wachezaji klabuni kwetu ni kocha mkuu Mr George Lwandamina na timu yake sio kiongozi mwingine yoyote na kocha huyo hajatoa taarifa yoyote ya kumwacha mchezaji gani au yupi kumuongezea mkataba zaidi ya kila siku kuukazania uongozi kuboresha masilahi yao kwa sababu kama kocha mkuu anajivunia na kujali kazi ya vijana wake.
Mwisho katibu mkuu anasisitiza kama klabu malengo yao makubwa ni kutetea ubingwa wa ligi kuu na watendaji wakuu ni wachezaji na benchi la ufundi hivyo wajikite zaidi katika hilo na wao kama uongozi kuhakikisha masuala ya kiutawala yapo sawa.
Imetolewa na kitengo cha habari na mawasiliano
Young Africans Sports Club.
02/05/ 2017
Young Africans Sports Club.
02/05/ 2017
Post a Comment