VIONGOZI WA MBAO FC WATOA PONGEZI KWA WACHEZAJI WAO

Uongozi wa timu ya soka ya Mbao FC,umewapongeza wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi kwa kucheza kwa juhudi kubwa na kufanikiwa kuipeleka timu kwenye fainali ya FA kwa mara ya kwanza.

Msemaji wa timu hiyo,Christian Malinzi alisema kwamba haikuwa kazi rahisi kwa timu ya Mbao FC kuiondosha Yanga ambayo kiuhalisi ni moja ya timu kongwe na yenye uzoefu mkubwa tofauti na wao ambapo wamepanda daraja msimu huu.

Katika hatua nyingine Malinzi ameizungumzia fainali yao watakayocheza na wekundu wa Msimbazi Simba,ambapo amesema kwamba kwa upande wao washaanza maandalizi kwa ajili ya fainali hiyo.

Malinzi alisema kwamba anaamini fainali hiyo itakuwa na ushindani mkubwa lakini kwa upande wao wamedhamiria kuibuka na ushindi kwenye pambano hilo ili wapate tiketi ya kucheza michuao ya kimataifa kwa ngazi ya vilabu.

Hata hivyo amewatoa hofu mashabiki na wadau wa mpira wa miguu kuwa endapo kama Mbao watapa nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa kwao hawataweza kuteteleka kwani wamejipanga vyema kwa ajili ya mashindano hayo.

No comments