CHECHE;SIMBA ILISHINDA KWA MIPANGO YA WAAMUZI

Kocha msaidizi wa timu ya Azam FC,Idd Cheche amelaamu maamuzi ya waamuzi waliochezesha mchezo wao wa nusu fainali ya FA dhidi ya Simba kwa kusema kwamba waamuzi hao wameshindwa kutafasiri sheria 17 za soka na kusababisha kikosi chake kufungwa kwa jumla ya bao 1-0.

Cheche alisema kwamba ameshangazwa na kadi nyekundu ya mapema iliyotolewa kwa mchezaji wake Salum Abubakar,ambapo amedai kuwa kadi hiyo imetolewa kimakosa ili kuilinda timu pinzani.

"Sisi tulijua jambo hilo tangu mapema na tuliwaambia wachezaji wetu sababu hii hali tuliona kwamba mchezo utakuaje, na wenyeji wa ligi ya Tanzania wanajua, hatutaki kwenda mbali zaidi lakini wale ambao wanaufuatilia mpira toka miaka ya 70 kuja juu wanajua hii hali,sasa nafikili kadi ilitoka ya mepema tena ya mojakwamoja ilituumiza zaidi"alisema Cheche.

Aidha alisema kwamba mbali na kadi hiyo lakini pia kumekuwa na makosa mengi ambayo wameyafanya waamuzi hao yaliyopelekea kuwadhohofisha wachezeji wake kwani kuna makosa ya wazi yalionekana.

Hata hivyo alisema kwamba kwa sasa baada ya kushindwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa wanarejea kujipanga upya kwa ajili ya mwakani.


No comments