JAMBELE;YANGA KUNA MPASUKO WA UONGOZI

Aliyewai kuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika uongozi wa klabu ya Yanga,John Jambele amedai kuwa ndani ya uongozi wa Yanga kwa kipindi hiki kumegawanyika makundi mawili ambalo kila kundi linafanya mambo yake.

Jambele alisema kwamba kutokana na mfumo huo klabu ipo kwenye wakati mgumu wa kutetea ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu kwani hakuna maelewano mazuri kwa viongozi hao.

Alisema kwamba hata kufungwa kwao na timu ya Mbao FC kwenye mchezo wa kombe la FA kulionekana wazi tangu mapema kwani kulikuwa na mkanganyiko wa safari,wengine wakienda Dodoma huku kundi linginene likienda Mwanza.

"Ndugu yangu mwandishi pale Yanga uongozi umegawanyika makundi mawili kuna kundi la kina Mkemi ambalo nalo linafanya mambo yake na kundi lingine,mfano ile safari ya Dodoma hivi kuna kiongozi gani alitoa maelezo juu ya safari hiyo na kwa nini kulikuwa na mvurugano"alisema Jambele.

Aidha alisema kwamba endapo kama uongozi wa timu hiyo kwa kipindi hiki hautakaa pamoja kufanya maswala yao kwa weledi anaamini Yanga haitakuwa bingwa wa ligi kuu kwa msimu huu kwani bado wana kazi kubwa ya kufanya.

Hata hivyo MWANDIKE.BLOGSPOT ilifanya jitihada ya kuzungumza na mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Yanga Salum Mkemi ili kubaini jambo hilo,ambapo kwa upande wake alisema kuwa ndani ya timu hiyo hakuna mgawanyiko wowote wa uongozi.

No comments