SIMBA KUWASILISHA MALALAMIKO YAO FIFA

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kwa sasa wanasubiri barua kutoka bodi ya ligi ili wawasilishe malalamiko yao katika shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Raisi wa klabu hiyo Evansi Aveva amesema kwamba wameamua kufanya hivyo baada ya kupokwa pointi tatu na kamati ya TFF licha ya kuwa na haki ya kupata pointi hizo.

Alisema kwamba mbali na swala hilo la kupokwa pointi tatu lakini pia watawasilisha maswala mbalimbali ambayo TFF wameshindwa kuyapatia ufumbuzi ikiwemo swala mchezaji wao Mbraka Yusuph anaekipiga kwenye klabu ya Kagera Sugar.

Aidha Aveva alisema kwamba anashangaa kuona wanashindwa kupata haki yao juu mchezaji Mbaraka Yusuph ilihali klabu hiyo ina mamlaka yote ya kummiliki mchezaji huyo anaefanya vizuri kwenye kikosi cha Kagera Sugar kwa msimu huu kwani alienda huko kwa mkopo.

No comments