FAINALI YA FA KUPIGWA MKOANI DODOMA

Mechi ya fainali ya kombe la FA itakayowakutanisha wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza sasa rasmi itapigwa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma siku ya tarehe 28 ya mwezi huu.

Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,Jamali Malinzi alisema kwamba mechi hiyo itachezwa mkoani Dodoma kufuatia uwanja wa Taifa uliopo jijini Dar es salaam kufungwa kuanzia may 21 kwa ajli ya kupisha upandaji wa nyasi mpya kwenye uwanja huo.

"Kwa mujibu wa mkandarasi anasema muda atakaoitaji kufanya hiyo kazi lazima hiyo kazi aianze baada ya tarehe 21 kwa hiyo tarehe 28 uwanja hautapatikana kwa ajili ya mchezo huo,kwa hiyo hata droo haina maana yeyote kwa sasaba kama uwanja wa Taifa haupo, upo wa CCM Kirumba haina maana ya kufanya droo"alisema Malinzi.

Malinzi ameongeza kuwa pia fainali hiyo kuchezwa mkoani Dodoma kunaleta tija kwa wakazi wa Dodoma hasa kwa kipindi hiki ambacho Serikali imeazimia kuhamishia makazi yake mkoani humo.

No comments