TFF WAUKATAA MFUMO WA UKODISHWAJI NDANI YA KLABU YA YANGA
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limesema
kwamba kwa sasa bado hawatambui mabadiliko yaliyofanyika ndani ya klabu ya
Yanga ya mfumo wa kukodisha timu kwa muda wa miaka 10 kwa kampuni iliyopewa
jina la Yanga yetu.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii katibu mkuu
wa TFF,Mwesigwa Selestine amesema kwamba kwa mujibu wa taratibu za klabu ya
Yanga TFF inaendelea kutambua mfumo wa awali wa uendeshaji na sio huu
unaozungumzwa na vyombo mbalimbali vya habari kwani bado shirikisho hilo
halijapelekewa barua inayoelezea mabadiliko hayo.
Amesema kwamba Yanga ni klabu ya wanachama hivyo kile
ambacho kinapaswa kufanyiwa marekebisho ni vyema kifuate misingi na katiba ya
klabu hiyo ili chini ya mwenyekiti Yusuph Manji.
Katika hatua nyingine Mwesigwa amesema kwamba shirikisho
hilo limeiandikia barua klabu ya Yanga ili kupata ufahamu wa jinsi mchakato wao
wa mabadiliko ulivyofanyika.
Mwesigwa amesema kwamba TFF imeomba nakala kwa katibu mkuu
wa klabu hiyo ili kufahamu vizuri mkataba wa ukodishwaji na waweze kuupitia ili
kama una mapungufu yaweze kufanyiwa kazi kwani Yanga ni klabu ya wanachama
hivyo mpangilio wa uendeshaji wa klabu ukiwa mbaya basi huenda kukawa na athari
kubwa kwa wanachama wa klabu hiyo.
Post a Comment