TFF YAIBUA UPYA UBUNIFU WA JEZI ZA TIMU ZA TAIFA

 
Shirikisho la soka nchini TFF limetoa ufafanuzi wa kina kuhusu mchakato wa ubunifu wa jezi za timu za taifa ambao umeachwa kwa wabunifu wa mavazi pamoja na wadau wengine hapa nchini.

Ofsa habari wa TFF Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kua mpango wa ubunifu wa jezi mpya za timu za taifa, umeibuliwa tena kutokana na mikakati iliyowekwa na uongozi uliopo madarakani chini ya Raisi wa shirikisho hilo Jamali Malinzi wa kuhakikisha kila inapopita miaka miwili lazima timu za taifa ziwe katika mtazamo tofauti kimavazi.

Alfred amesema suala hilo wamemaua kulifanya kuwa wazi kwa kila mdau kushiriki kikamilifu ili kupata muundo na muonekano mzuri wa jezi ambazo zitaanza kutumika mwaka ujao.

No comments