KISA UKATA WA FEDHA SHIMBATA YASHINDWA KUMUENZI NYERERE

Raisi wa shirikisho la mchezo wa bao hapa nchini [SHIMBATA] Mondy Likwepa amesema kwamba shirikisho hilo limeshindwa kumuenzi baba wa taifa mwalimu Julias Kambarage Nyerere katika siku ya kumbukumbu ya kifo chake iliyofanyika jana kutokana na shirikisho hilo kukabiliwa na ukata mkubwa wa fedha.

Likwepa amesema kwamba shirikisho hilo halikuungwa mkono na wadau mbalimbali ili kufanikisha shindano la kuenzi kumbukumbu ya kifo chake kwani kumekuwa hakuna vifaa vyovyote ambavyo vingefanikisha shindano hilo.

Amesema mbali na kushindwa kufanikisha jambo hilo lakini kwa kutambua umuhimu wa Baba wa Taifa hasa katika mchezo wa bao wamepanga kuendelea kumuenzi kwa njia mbalimbali na wanataraji kufanya shindano siku ya tarehe 19 ya mwezi wa 11 mwaka huu na hii kwa ajili ya kuendelea kumuenzi.

No comments