RUVU SHOOTING WATAMBA KUIFUNGA MBEYA CITY

Baada ya kulazimishwa sale ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ndanda katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa uwanja wa Mabatini,leo hii uongozi wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani umesema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mechi yao watakayocheza na Mbeya City hapo kesho

Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba matokeo waliyoyapata mbele ya Ndanda yamewahudhunisha kwani haikuwa dhamira yao kuona wanapata alama moja tena wakiwa nyumbani.

"Nadhani mechi yetu dhid ya Ndanda ingekuwepo kwenye mpangilio wa kubeti basi idadi kubwa ya watu wangeipa pointi timu yetu ya Ruvu Shooting hivyo kwa sasa hatutaki kuwaangusha"alisema Masau.

Amesema mikakati iliyopo kwa sasa ni kuona wanapata ushindi mbele ya Mbeya City ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya msimamo wa ligi.

No comments