BAADA YA BMT KUTOTAMBUA UKODISHWAJI,YANGA WAITISHA MKUTANO MKUU WA DHARURA KWA MARA NYINGINE


Uongozi wa klabu ya Yanga umeitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama unaotaraji kufanyika siku ya jumapili ya tarehe 23/10/2016.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika klabu hiyo zinasema kwamba mahala utakapofanyika mkutano huo na agenda za mkutano,uongozi utaweka wazi hapo baadae kabla ya siku husika ya mkutano mkuu wa dharura.

Aidha uongozi huo wa Yanga umewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo kwani kufika kwao kutaleta maslahi mapana ya ndani ya klabu hiyo.

Itakumbukwa kwamba huu ni mkutano wa pili wa dharura kwa mwaka huu ndani ya klabu hiyo ambapo awali kulifanyika mkutano kama huo ambao wanachama kwa pamoja waliridhia timu ikodishwe kwa muda wa miaka kumi kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji.

Huenda mkutano huo ukalenga hoja ya ukodishwaji wa timu hiyo na hii inatokana na serikali kupitia kwa baraza la michezo Tanzania BMT kusema kwamba hawatambui ukodishwaji uliofanywa na viongozi wa Yanga kwa kampuni ya Yanga Yetu kwakua ukodishwaji huo haukufuata misingi ya katiba ya klabu.

No comments