MWAISABULAH AMKINGIA KIFUA KOCHA HANS



Mchambuzi wa mpira wa miguu hapa nchini Kenny Mwaisabulah amesema kwamba uongozi wa Yanga utafanya kosa kubwa endapo utachukua jukumu la kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi kwani kwa sasa makocha hao wanapaswa kusalia ndani ya klabu hiyo iliyoingia kwenye mchakato wa mabadiliko ya kiutawala.

Mwaisabulah amesema kwamba kwa sasa benchi la ufundi la Yanga ni vyema likaendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwani kwa muda mrefu wamekaa pamoja na wachezaji na hata kiwango chao cha ufundishaji bado kinaridhisha.

Amesema kwamba huenda uongozi wa Yanga ukafanya jambo hilo baada ya kutopata matokeo mazuri katika pambano lao la watani wa jadi dhidi ya Simba lakini kwa mtazamo wake makocha hao bado wana mchango mkubwa ndani ya timu na kwake haoni makosa yanayofanywa na makocha hao hasa kocha mkuu anayenyoshewa kidole na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo.

No comments