RAGE AWAPONGEZA VIONGOZI WA SIMBA KWA KUFANYA USAJILI MZURI

Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba,Ismail Aden Rage amesema kwamba ushirikiano uliopo baina ya viongozi, wachezaji pamoja na wanachama wa klabu hiyo ndio chachu kubwa ya timu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Rage amesema kwamba mbali na ushirikiano huo pia uongozi umefanikiwa kufanya usajili mzuri ambao kila mchezaji anaonyesha kiwango bora pale anapopata nafasi ya kucheza.

Amesema kwamba kwa sasa ni mapema kuitabilia timu hiyo kuchukua ubingwa kwani ligi ndio kwanza ipo katika mzunguko wa kwanza lakini endapo kama wataendelea na kasi hii ambayo wameanza nayo basi matumaini ya kuchukuwa ubingwa ni mkubwa.

"Kuhusu kuwa mabingwa kwa sasa ni mapema mno lakini wakijizatiti wanaweza kutimiza ahadi yao lakini viongozi wamefanya usajili mzuri na wameonyesha nia ya kusaka mataji msimu huu"alisema Rage.

No comments