UONGOZI WA YANGA WAKANUSHA TAARIFA ZA KUJIUZULU KWA MANJI

Huku kukiwa na taarifa kuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji yuko mbioni kujiuzulu wazifa huo Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba taarifa za kujiuzulu  si za kweli kwani bado anaendelea na majukumu yake ya kiutawala ndani ya timu hivyo ni vyema mashabiki wakaondoa hofu juu ya jambo hilo ambalo halina ukweli wowote.

Kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deusdedit amesema kwamba pia uongozi huo umepokea barua kutoka TFF ikihitaji klabu hiyo kuwapatia nakala ya mkataba wa mfumo mpya wa mabadiliko kilichopo kwa sasa ni wao kutekeleza jambo hilo.

"Hizo taarifa si za kweli na pia wanachama wanapaswa kuamini taarifa ambazo zinazothibitshwa na uongozi kwani mara nyingi taarifa zinazoandikwa kwenye mitandao hazina ukweli"alisema Baraka.

Amesema nakala hiyo ya mkataba wa mfumo mpya wa utendaji baada ya timu kukodishwa kwa miaka 10 kwa kampuni ya Yanga yetu itapelekwa baada ya mkutano mkuu wa dharula unaotaraji kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

No comments