UONGOZI WA JKT RUVU WAKILI KUWA SAFU YA USHAMBULIAJI YA TIMU HIYO BUTU

Uongozi wa timu ya soka ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani umesema kwamba kwa sasa kocha mkuu wa klabu hiyo Malale Hamsini anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu ambayo yameonekana ndani ya kikosi cha timu hiyo ili kiweza kufanya vizuri katika michezo ya ligi inayofuata.

Katibu mkuu wa klabu hiyo Ramadhani Madoweka ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba mwalimu mkuu amegundua mapungufu kwenye nafasi ya ushambuliaji ambayo inawafanya washindwe kuchomoza na ushindi licha ya kucheza wakiwa nyumbani.

"Tumezungumza na mwalimu kuhusu hilo jambo na yeye ametuambia kuwa kuna mapungufu kwenye nafasi ya ushambuliaji kwani wachezaji wa nafasi hiyo huwa hawapo makini wanapokuwa langoni mwa timu pinzani hivyo ametuambia kuwa anayafanyia kazi"alisema Madoweka.

Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo umesema kwamba unaamini utafanya vizuri katika pambano lao la kesho dhidi ya Mwadui kwani wanaamini marekebisho ambayo anayafanya kocha mkuu yatakuwa na tija kwa upande wa kikosi hicho.

No comments